Japan yazindua kifaa maalum cha kuwatambua wanyanyasaji wa kingono

Japan yazindua kifaa maalum cha kuwatambua wanyanyasaji wa kingono

Like
947
0
Friday, 30 August 2019
Global News

Kifaa kilicho na muhuri maalum wa kuwatambua wanyanyasaji wa kingono katika magari ya usafiri wa umma kimezinduliwa nchini Japan.

Kifaa hicho kinamfahamisha muathiriwa kuwa kuna mtu anampapasa na kuwawekea alama ya wino ambayo hauonekani.

Watu wanaweza kuwatambua wanyanayasaji wa kingono waliowekwa alama hiyo kwa kutumia taa nyeusi kuwabaini.

Wasafiri wakiwa ndani treni

Shirika la kiteknolojia lililobuni kifaa hicho linasema kiitasaidia kukabiliana na uhalifu wa kingono.

Hata hivyo shirika moja lisilokuwa na kiserikali linanahofia kifaa hicho kinaweza kutumika vibaya na watu wenye chuki dhidi ya watu fulani.

Kampuni Japani linalofahamika kama hachihata linasema liliamua kutengeza muhuri huo ili kuwadhibiti watu wanaowanyanyasa kingono abiria katika vituo vya treni.

Kampuni hiyo ilitangaza wazo la kubuni muhuri huo mara ya kwanza mwezi wa tano baada ya video inayowaonesha wasichana wawili wa Japan wakimkimbiza mshukiwa wa unyanyasaji wa kingono katika kituo cha usafiri wa treni iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii kupata umaarufu.

Msemaji wa kapuni ya Shachihata aliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa kifaa hicho”ni hatua moja kuelekea ulimwengu usiokuwa na uhalifu wa kingono”.

Wasafiri wakiingia ndani treni mjini Tokyo

Lakini msemaji wa kitengo ckinachoshughulikia masuala ya ubakaji England na Wales ameiambia BBC huenda kifaa hicho kikatumiwa kibiasha na kufanya kuwa rasmi masuala ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono na kuwaeka hatarini wale wanaomiliki kifaa hicho.

“Japo waliobuni kifaa hicho wamekitengeza kwa nia njema nahofia pia kunawatu watakaotumia kujifaidi- kutokana na waathiriwa wa ubakaji’,” anasema Katie Russell.

Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni zaidi kufikiwa katika majaribio ya kukabiliana na visa vya upapasaji nchini humo, ikiwa ni miezi michache tu baada ya kuzinduliwa kwa programu inayojulikana kama Digi Police, inayolinda waathirika dhidi ya visa vya unyanyasaji katika maeneo yenye msongamano wa watu.

Kifaa hicho kinawafahamisha abiria wengine kwamba wako hatarini kwa kuonyesha ujumbe unaosema: “Kuna mtu anayepapasa watu hapa. Tafadhali nisaidie.” Kamera za kukabiliana na visa vya upapasaji ziliwekwa kwenye treni za jiji la Tokyo mwaka 2009 kusaidia kukabiliana na malalamiko ya unyanyasaji wa kingono.

Zaidi ya watu 6,000 walikamatwa kwa kushukiwa kutekeleza vitendo hivyo mwaka huohuo.

Harakati zinazoendeshwa na vuguvugu la #MeToo bado hazijafanikiwa nchini Japani ambayo inaorodheshwa kuwa nambari 110 katika nchini 149 kwenye suala la usawa wa kijinsia katika kipimo cha Kongamano la Kiuchumi Duniani.

 

 

 

cc:BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *