JORDAN YAAHIDI KUOKOA MAISHA YA RAIA WAKE ANAESHIKILIWA NA IS

JORDAN YAAHIDI KUOKOA MAISHA YA RAIA WAKE ANAESHIKILIWA NA IS

Like
220
0
Monday, 02 February 2015
Global News

SERIKALI ya Jordan imesema  imedhamiria kutumia kila njia kuyaokoa maisha ya raia wao anaeshikiliwa na wafuasi wa itikadi kali wa dola ya kiislam IS. Habari hizo zimetangazwa na shirika la habari la Jordan-Petra.

Hapo Jana wanamgambo hao wa IS walimuonyesha katika kanda ya video mwandishi wa habari wa Japan Kenji Goto waliyemkata kichwa Serikali ya Japan imesema kanda hiyo ni ya kweli.

Hapo awali wafuasi hao wa itikadi kali walionya watawauwa mahabusi wote wawili wa Japan ikiwa serikali mjini Amman haitomwachia huru mwanaharakati wao wa kike,hadi usiku wa alhamisi iliyopita.

 

Comments are closed.