Je chama cha Kijani Ujerumani ni chama kipya cha umma?
Lakini sasa wanakijani wamepevuka na yumkini wako tayari kuyatekeleza majukumu ya vyama vikubwa vya umma. Kilipoingia bungeni kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1986 na msimamo mkali wa kutetea mazangira chama cha kijani kiliutikisa mfumo wa siasa ya vyama vikubwa vya umma nchini uliyoibuka baada ya kumalizika vita vikuu vya pili.
Miaka 35 tangu wakati huo chama cha kijani kimekomaa. Wanachama wake sasa wanavaa suti na wanafunga tai pia wameachana namsimamo mkali wa kulinda mazingira na badala yake wanaendesha siasa inayofuata uhalisia wa mambo. Wanatekeleza siasa halisi ya kuzingatia mabadiliko ya kidijitali na sera ya utangamano wa kijamii.
Wajumbe wa chama cha kijani wamo katika serikali za majimbo 11 ya Ujerumani na hali hiyo imekifanya chama hicho kishike nafasi ya pili katika uchaguzi uliofanyika kwenye jimbo la Bavaria la kusini mwa Ujerumani.
Licha ya utabiri kwamba huenda chama cha kijani kikageuka kuwa chama kikubwa cha umma, kurejea kwake katika umaaruufu kunaashiria kipindi cha mfarakano wa vyama vikuu vya siasa. Hali hiyo inaweza kuvinufaisha vyama vya Kijani na kile cha mrengo mkali wa kulia, (AfD) kinachopinga wanamiaji, vyama ambayvo hadi hivi karibuni vilikuwa vimesimama kandoni mwa siasa kuu za nchini. Vyama hivyo viwili vinanufaika na udhaifu uliomo katika vyama vikuu vya umma, vya CDU na SPD.