Je Mugabe atamrithisha mkewe mamlaka?

Je Mugabe atamrithisha mkewe mamlaka?

Like
422
0
Monday, 29 September 2014
Global News

 

 

 

 

 

 

MUGABE

Rais Mugabe akiwa na mkewe bi.Grace Mugabe

Hivi karibuni kumekuwa na swali ambalo linawatatiza watu wengi hususani raia wa Zimbabwe kufuatia mtukio ya rais wa nchi hiyo kumkabidhi mkewe nyazfa mbalimbali za juu kiutawala.

Kuzaliwa kwa utawala wa kinasaba sio jambo jepesi kubashiri.

Lakini wananchi wengi wa Zimbabwe kwa sasa wanaonekana kushawishika kuwa kuna uwezekano wa familia ya Mugabe kuingia katika orodha hiyo ya kurithishana madaraka.

Rais Mugabe ana umri wa miaka 90. Mke wake, Grace, ana umri wa miaka 49.

Uvumi wa kurithishana madaraka umekuwa gumzo la kisiasa nchini Zimbabwe kwa miaka mingi, lakini Grace Mugabe katika miaka ya karibuni ameibuka kama mtu ambaye ataweza kumrithi mumuwe madaraka ya uongozi wa nchi ya Zimbabwe.

Watu wa nje wamesikia tabia ya mke wa Rais Mugabe ambaye ni karani muhtasi wake wa zamani kutuhumiwa kufanya manunuzi yasiyo na mpangilio na katika tukio lingine kumpiga ngumi mwandishi wa habari wa Uingereza huko Hong Kong; na kufanya mambo mengine ambayo yanavuka mpaka kama mke wa kiongozi.

Vyombo vya habari vya Zimbabwe, kwa kulinganisha vimedhamiria kumjenga Bi Grace Mugabe kuwa mtu wa kujitolea kwake katika kazi za kijamii.

 

MUGABE2

“Wakati mume wake akiondoka ndiyo mwisho wake wa kazi ya uanasiasa, kama kweli kuna kazi ya aina hiyo” anasema mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Zimbabwe,anasema Ibbo Mandaza, akitupilia mbali wazo la kuendelea kuwa na utawala wa familia ya Mugabe.

Nadharia nyingine ni kwamba Rais Mugabe anamjenga mke wake ili kuyayumbisha makundi yote ndani ya chama cha Zanu-PF, na kuimarisha nafasi yake ya urais.

Dewa Mavhinga, kutoka Human Rights Watch, anaamini kuwa rais amefanya kosa kubwa kumleta mtu ambaye hana ujuzi wowote wa siasa.

“Inaonyesha kuwa Rais Mugabe hamwaamini mtu yeyote karibu naye”Dewa Mavhinga.

 

 

 

Comments are closed.