Jean-Pierre Bemba azuiwa kugombea urais na mahakama DRC

Jean-Pierre Bemba azuiwa kugombea urais na mahakama DRC

Like
494
0
Tuesday, 04 September 2018
Global News

Mahakama ya juu kabisa ya kikatiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema kiongozi wa upinzani , Jean-Pierre Bemba, hana sifa ya kuwa rais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kiongozi huyo amezuiwa kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Macho sasa na masikio yote yameelekezwa kwa Bemba ambaye anaishi uhamishoni mjini Brussels endapo ataamua kumuunga mkono mgombea mwingine kutoka kambi ya upinzani .

Ingawa mpaka sasa wagombea wote kutoka kambi ya upinzani wanaonekana kutokuwa na sifa ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo na kuufanya uchaguzi huo kujaa maswali mengi kuliko majibu endapo utakuwa huru na wa haki kwa mgombea wa chama tawala kusimama pekee kwenye uchaguzi huo ambao umeahirishwa kwa miaka miwili mpaka kufikia sasa.

Bwana Bemba, ambaye anatajwa kama mpiganaji wa zamani, aliyewahi pia kushika wa dhifa wa makamu wa raisi nchini DRC , Bemba alikosa sifa za kustahili kusimama na kugombea nafasi hiyo kutoka na sababu mojawapo inayotajwa kuwa ni hukumu iliyotolewa na mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa madai ya kuwahonga mashahidi .

Hivi karibuni Bemba hivi karibuni aliachiliwa katika kesi dhidi ya uhalifu wa kivita na mahakama baada ya kutumkia miaka kumi jela.

Mwezi uliopita alirejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kupokelewa kwa mapokezi makubwa kutoka kwa wafuasi wake.

JEAN-Pierre Bemba anatajwa kama mpinzani namba moja anayesumbua kichwa cha Joseph Kabila katika uchaguzi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *