JENERALI SEJUSA AFIKISHWA MAHAKAMANI

JENERALI SEJUSA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Like
226
0
Tuesday, 02 February 2016
Global News

JENERALI mwenye utata nchini Uganda David Sejusa amewasili katika mahakama moja ya kijeshi katika mji mkuu wa Kampala nchini Uganda tayari kujibu mashitaka yanayomkabili ambayo hata hivyo bado hayajawekwa hadharani.

Siku ya jumatatu chombo cha habari cha Bloomberg kilimnukuu msemaji wa serikali Ofwono Opondo akisema kuwa Uganda inachunguza ripoti zinazomuhusisha jenerali mtoro David Sejusa na makundi yenye mipango ya kuzua ghasia.

Jenerali Sejusa aliwekwa katika kifungo cha nyumbani siku ya jumapili mjini Kampala.

Comments are closed.