JESHI LA POLISI LAWATAKA WANASIASA KUZINGATIA SHERIA NA MIONGOZO YA NEC

JESHI LA POLISI LAWATAKA WANASIASA KUZINGATIA SHERIA NA MIONGOZO YA NEC

Like
251
0
Monday, 21 September 2015
Local News

IKIWA Zimebaki siku 33 kufika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani, Jeshi la polisi nchini limewataka viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia sheria zinazowaongoza na miongozo mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Ili Kuhakikisha Uchaguzi mkuu unakuwa wa Amani.

Akizungumza na kituo hiki Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini-SSP-ADVERA BULIMBA Amesema Kuwa ili kulinda amani iliyopo nchini hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu Wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi hawana budi kujiepusha na vitendo vinavyoonesha uvunjifu wa Amani.

Aidha ametoa wito kwa watanzania kuliamini Jeshi la polisi kwani Litahakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu unakuwa Huru na Amani na kuto ruhusu mtu yoyote kufanya vurugu ambazo zitaharibu Amani ya Nchi.

Comments are closed.