JK AANZA ZIARA ZAMBIA

JK AANZA ZIARA ZAMBIA

Like
242
0
Wednesday, 25 February 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka leo kuelekea Lusaka Zambia kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku mbili kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais Edgar Chagwa Lungu wa Nchi hiyo.

Viongozi hao wanatarajia kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hizi ikiwemo suala la reli ya Tanzania na Zambia Railway Authority (TAZARA), inayounganisha Tanzania na Zambia.

Hivi karibuni Reli ya TAZARA imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitajika kujadiliwa kwa kina na viongozi wakuu ili kuimarisha zaidi reli hiyo ambayo ni kiungo kikubwa baina ya nchi hizi katika masuala ya uchumi na alama ya ushirikiano.

Comments are closed.