JK AWAASA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII

JK AWAASA WANAFUNZI KUSOMA KWA BIDII

Like
317
0
Tuesday, 24 February 2015
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE amewaasa wanafunzi wa shule zote za sekondari nchini kusoma kwa bidii masomo yote hususani ya sayansi ili kuinua kiwango cha elimu na kuliletea Taifa maendeleo.

Rais KIKWETE ametoa wito huo leo wakati akipokea rasmi vitabu milioni mbili na laki tano vya sayansi na hisabati katika shule ya sekondari ya MTAKUJA BEACH Kunduchi jijini Dar es salaam kutoka kwa serikali ya marekani kupitia shirika la msaada la-USAID- kwa lengo la kusaidia shule za sekondari za serikali kote nchini.

Katika makabidhiano hayo Rais KIKWETE amesema kuwa mbali na mafanikio na changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya elimu serikali imejidhatiti ipasavyo kuhakikisha kuwa elimu inakua kwa kiwango kikubwa kwa kuboresha huduma ikiwemo mishahara ya walimu.

 

Comments are closed.