WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry amesema iwapo Marekani itajitoa kutoka katika makubaliano ya nyuklia na Iran na kutaka washirika wake watekeleze hatua za vikwazo vya Marekani, kutakuwa na kitisho cha kupotea imani na uongozi wa Marekani pamoja na kupoteza mwelekeo wa sarafu yake ya dola.
Akitetea makubaliano ya Julai 14 yaliyoafikiwa mjini Vienna kati ya Iran na mataifa makubwa yenye nguvu duniani, Kerry ametoa utetezi mpya katika mapambano kuwazuia wabunge wa Marekani kuvunja makubaliano hayo.