Licha ya Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Umande Chama kutangaza kuwa Mwamuzi wa pambano la watani wa jadi atatangazwa Alhamis ya wiki hii, taarifa za ndani zinasema Jonesia Rukiyaa atachezesha pambano hilo.
Imeelezwa kuwa Rukiyaa atashika filimbi katikati ya Uwanja huku akisaidiana na Ferdnand Chacha pamoja na Mohammed Mkono.
Aidha, chanzo hicho kimesema Mwamuzi wa mezani atakuwa ni Elly Sasii.
Jana ilielezwa pia kuwa Mwanamama Florentino Zabron kutoka Dodoma angechezesha mechi hiyo lakini kumefanyika mabadiliko tena mengine.
Kikao cha Kamati ya Waamuzi na Wanahabari kinatarajiwa kukutana kesho kunako Makao Makuu ya Shirikisho la Soka mitaa ya Ilala Karume, ili kuweka bayana zaidi juu ya Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo.
Tayari Simba na Yanga wameshaanza kambi kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.