JOTO LA KLABU BINGWA BARANI ULAYA

JOTO LA KLABU BINGWA BARANI ULAYA

Like
338
0
Thursday, 06 November 2014
Slider

Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona, Lionel Messi afikia rekodi ya magoli 71 ndani ya michuano ya klabu bingwa Ulaya iliyokuwa inashikiliwa na legendari Raul Gonzalez.

Messi amefikia rekodi hiyo baada ya kufanikiwa kupachika magoli mawili katika mchezo dhidi ya Ajax Amsterdam kwa kuisadia klabu ya Barcelona kupata ushidi wa magoli mawili kwa sifuri na kukata tiketi ya kutinga raundi ya 16 bora.

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Real Madrid na S04, Raul ilimchukua takribani michezo 142 kuweza kufikisha idadi ya magoli 71 ila imemchukua jumla ya mechi 90 tu kwa nahodha wa Argentina, Lionel Messi kufikia mafanikio hayo.

Messi na Ronaldo mwenye magoli 70 wanachuana kuweza kufikisha magoli 72 na kuweka rekodi mpya katika michuano hiyo ila Muargentina huyo ana nafasi kubwa zaidi ya kuweza kufikisha idadi hiyo pale Barcelona watakapochuana na klabu ya Apoel Nicosia mnamo tarehe 25 mwezi wa 11 mwaka 2014 kabla ya Ronaldo na kikosi cha Real hakijashuka dimbani kesho yake dhidi ya FC Basel.

Comments are closed.