JUMUIYA YA KIMATAIFA YAONYWA KUTOLEGEZA KAMBA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA EBOLA

JUMUIYA YA KIMATAIFA YAONYWA KUTOLEGEZA KAMBA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA EBOLA

Like
258
0
Wednesday, 05 November 2014
Global News

AFISA wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mapambano dhidI ya maradhi ya Ebola, ameionya jumuiya ya kimataifa isilegeze kamba katika harakati za kuyatokomeza maradhi hayo hatari.

Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf mjni Monrovia, afisa huyo Anthony Banburry amesema ingawa zipo dalili za kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo, kila mtu anapaswa kuendelea kuwa makini.

Banburry amesema Umoja wa Mataifa umejenga vituo vya kupambana na Ebola, na inahitaji watu wa kujitolea kuviendesha vituo hivyo. Wakati huo huo, Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola yameonyesha matumaini ya mafanikio.

 

Comments are closed.