MAREKANI KUPELEKA RASIMU YA VIKWAZO UMOJA WA MATAIFA

MAREKANI KUPELEKA RASIMU YA VIKWAZO UMOJA WA MATAIFA

Like
231
0
Wednesday, 05 November 2014
Global News

MAREKANI imesema itapeleka rasimu ya maazimio ndani ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka vikwazo dhidi ya Watu wanaozorotesha hali ya kisiasa nchini Sudani Kusini.

Rais wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Australia amesema baadhi ya wanachama wa baraza hilo wanaunga mkono hatua ya kuwekewa vikwazo na kuzuia biashara ya silaha.

Haijajulikana ni lini hatua hiyo itatekelezwa. Lakini Mapigano yameendelea nchini Sudani Kusini ,ingawa kumekuwa na jitihada za kimataifa kuhakikisha makubaliano ya amani yanatekelezeka.

Mzozo wa kuwania madaraka uliokuwepo kwa miezi kumi kati ya Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar umegharimu maisha ya maelfu ya Watu na takriban watu milioni mbili kuyakimbia makazi yao.

 

Comments are closed.