JUMUIYA YA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MTAKATIFU JOSEPH WAUNGANA KUCHANGIA DAMU

JUMUIYA YA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MTAKATIFU JOSEPH WAUNGANA KUCHANGIA DAMU

Like
279
0
Tuesday, 20 October 2015
Local News

JUMUIYA ya wanafunzi waliosoma shule ya sekondari ya Mtakatifu Joseph kwa wameungana na wanafunzi wa sasa wa shule hiyo kuichangia damu hospitali ya Taifa ya muhimbili ili kuwasaidia watanzania wenye mahitaji ya kuongezewa Damu.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wanafunzi wa jumuiya hiyo Mariam Zialo ameeleza kuwa wamefanya zoezi hilo pamoja na wanafunzi wa sasa wa shule hiyo baada ya kuona uhitaji mkubwa wa damu uliokuwepo katika hospitali hiyo.

Kwa upande mwingine mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka hosptali ya Taifa muhimbili Aminiel Buberwa ameonesha kufurahishwa na kitendo hicho na kwamba wanataria kupata chupa za damu 300 ambazo zitasaidia kuendesha shughuli mbalimbali za upasuaji hospitalini hapo.

Comments are closed.