KAGERA :AFISA MIFUGO ANUSURIKA KUFUKUZWA KAZI

KAGERA :AFISA MIFUGO ANUSURIKA KUFUKUZWA KAZI

Like
445
0
Tuesday, 15 March 2016
Local News

AFISA MIFUGO wa kata ya Kakunyu, wilayani Misenyi mkoani Kagera, Eric Kagoro amenusurika kufukuzwa kazi kwenye mkutano wa hadhara kutokana na sakata la kuruhusu ng’ombe 291 kulishwa kwenye ranchi ya mifugo ya Misenyi.

Tukio hilo limetokea jana baada ya Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kuhoji juu ya malalamiko aliyoyapata kutoka kwa wananchi kuwa Afisa huyo ndiye aliyeruhusu mifugo hao kuingia kwenye eneo hilo.

Katika mkutano huo Waziri Mkuu amewaasa watendaji wa kata na vijiji kutotumia nafasi zao kuleta migogoro baina ya watu wa nje na wananchi wanaowaongoza na badala yake watumie nafasi zao kutatua kero za wananchi.

Comments are closed.