KAIMU MKURUGENZI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD ASIMAMISHWA KAZI

KAIMU MKURUGENZI WA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD ASIMAMISHWA KAZI

Like
485
0
Wednesday, 23 December 2015
Local News

WAZIRI wa afya , maendeleo ya jamii jinsia, watoto na wazee mheshimiwa UMMY MWALIMU amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugezi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dokta Diwani Msemo ili kupisha uchunguzi wa kubaini iwapo mgongano wa kimaslahi umeathiri utendaji wa taasisi hiyo chini ya uongozi wake.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya afya leo, inaeleza kuwa dokta Msemo amesimamishwa kazi kutokana na sababu mbalimbali  kama vile kuwepo kwa manung’uniko mengi kutoka kwa wapokea huduma hususani katika taasisi ya saratani ya ocean road likiwemo suala zima la kuuziwa dawa hata zile ambazo wagonjwa wanatakiwa kuzipata kwa bei ya ruzuku ama kutolewa bure na serikali.

Comments are closed.