KAMANDA WA KUNDI LA LRA KUFIKISHWA ICC

KAMANDA WA KUNDI LA LRA KUFIKISHWA ICC

Like
263
0
Wednesday, 21 January 2015
Global News

KIONGOZI wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la Uganda, Lord’s Resistance  Army, LRA amekabidhiwa kwa wawakilishi wa Mahakama  ya Kimataifa ya ICC, na sasa ameshawasili mjini The Hague ambako atafunguliwa kesi.

Kiongozi huyo Dominic Ongwen atakabiliwa na mashtaka ya uhalifu  wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kundi la kigaidi la LRA kwa muda mrefu limekuwa linafanya vitendo vya kinyama katika nchi za  Afrika mashariki na kati. Ongwen alijisalimisha mwenyewe kwa majeshi ya Marekani katika  Jamhuri ya Afrika ya Kati,yanayosaidiana na majeshi ya Umoja wa   Afrika katika kuwasaka magaidi wa LRA.

Comments are closed.