KAMATI KUU YA CHADEMA KUKUTANA KESHO

KAMATI KUU YA CHADEMA KUKUTANA KESHO

Like
236
0
Wednesday, 21 January 2015
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA, kimeitisha Kikao cha Kamati kuu kitakachofanyika kesho ambacho kitatoa maazimio na maamuzi ya chama kuhusu maswala mbalimbali kwa mustakabali wa wananchi kwa ujumla.

Akizungumza na Wandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Afisa habari wa chama hicho Tumaini Makene, amesema kikao hicho pia kitajadili zoezi la uandikishwaji wa Daftari kudumu la wapiga kura.

Hata hivyo Makene amesema swala la Elimu ya Katiba pendekezwa ikiwemo elimu ya kura ya maoni na Taarifa ya Ukawa kuelekea uchaguzi Mkuu pia vitapewa kipaumbele katika kikao hicho.

 

Comments are closed.