VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUJITAMBUA NA KUACHA KUTUMIWA NA WANASIASA

VIJANA NCHINI WAMETAKIWA KUJITAMBUA NA KUACHA KUTUMIWA NA WANASIASA

Like
184
0
Wednesday, 21 January 2015
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kujitambua na kuacha kutumiwa na baadhi ya wanasiasa kuwa mtaji wao wa mafanikio katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutokana na kubainika kuwa idadi yao ni kubwa zaidi.

Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Dokta Valentino Mokiwa amesema kwa mujibu wa taarifa ya  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dokta  Albina Chuwa,  Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuwa vijana ni asilimia 34.7 ya watu wote nchini, lakini pia ndiyo wengi zaidi katika kundi la wale wenye umri kati ya miaka 18 hadi 100.

Ameongeza kuwa hatua hiyo inatokana na kukosa mwelekeo mzuri wa maisha na ufahamu wa kutosha juu ya mustakabali wa maisha yao ya baadaye hivyo kwa kutumia udhaifu huo, mwanasiasa yeyote amekuwa na uwezo wa kumtumia kijana kama mtaji wake wa mafanikio.

 

 

Comments are closed.