KAMATI BORA ZA KUDHIBITI UKIMWI ZAZAWADIWA PANGANI

KAMATI BORA ZA KUDHIBITI UKIMWI ZAZAWADIWA PANGANI

Like
450
0
Monday, 21 December 2015
Local News

SHIRIKA lisilo la kiserikali Wilayani Pangani la-UZIKWASA linalojishughulisha na kuziwezesha kamati za kudhibiti Ukimwi, limetoa zawadi kwa kamati bora za kudhibiti ukimwi Wilayani humo.

 

Katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Jaira, kata ya Madanga wilayani Pangani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Maendeleo wa Wilaya hiyo, Bi.Patricia Kinyange.

 

Akizungumza katika hadhara hiyo Bi. Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa kuzijengea uwezo kamati hizo ambazo zinafanya kazi kubwa kwa jamii.

sal2

Burudani ya ngoma ilikua sehemu ya tamasha hilo.

 

 

 

sa

 

Comments are closed.