KAMATI YA TANZANIA KWANZA NJE YA BUNGE MAALUM LA KATIBA IMEWATAKA WANANCHI WAISOME NA KUILEWA KATIBA

KAMATI YA TANZANIA KWANZA NJE YA BUNGE MAALUM LA KATIBA IMEWATAKA WANANCHI WAISOME NA KUILEWA KATIBA

Like
259
0
Monday, 02 February 2015
Local News

KAMATI ya Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum la Katiba imewataka Watanzania kutokubali kutafasiriwa katiba pendekezwa na Wanasiasa au kikundi chocchote na badala yake waisome na kuijua ikiwa ni pamoja na kufuatilia matangazo ambayo Serikali inayatangaza.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Kwanza AGUSTINO MATEFU amesema kuwa kuna baadhi ya kikundi cha watu wachache ambacho kimevaa uhusika kwa ajili ya kuwataka waislam wasipigie kura katiba pendekezwa kwa kuwa hakuna kipengele cha Mahakama ya kadhi.

Aidha amesema kuwa tayari wameshaongea na Shekh mkuu wa Tanzania Shaban Bin Simba ambaye amesema kuwa halitambui kundi hilo.

Comments are closed.