KENYA: WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU MASHTAKA YA MAUAJI

KENYA: WAWILI WAPANDISHWA KIZIMBANI KUJIBU MASHTAKA YA MAUAJI

Like
215
0
Thursday, 28 January 2016
Global News

MAHAKAMA Kuu mjini Mombasa imeamua kwamba washukiwa wawili walioshitakiwa kwa mauaji ya watu 60 eneo la Mpeketoni miaka miwili iliyopita wana kesi ya kujibu.

Jaji Martin Muya amesema upande wa mashitaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kuwafungulia mashitaka wawili hao.

Diana Salim Suleiman na Mahadi Suleiman Mahadi ajulikanaye kama Jesus wanadaiwa kuhusika katika uvamizi uliopelekea kuuawa kwa watu 60 mwezi Juni mwaka 2014 katika vijiji vya Mpeketoni na Kaisairi, Kaunti ya Lamu.nchini Kenya.

 

Comments are closed.