Kim aahidi ‘historia mpya’ ya Korea mbili

Kim aahidi ‘historia mpya’ ya Korea mbili

Like
633
0
Friday, 27 April 2018
Global News
Rais w a Korea kaskazini Kim jong un na mwenzake wa Kusini Moon Jae-in

Rais w a Korea kaskazini Kim jong un na mwenzake wa Kusini Moon Jae-in

Kim Jong-un ameahidi ‘historia mpya’ katika uhusiano na jirani yake wakati akiwa kiongozi wa kwanza wa Korea kaskazini kuingi Korea ksuini tangu kumalizika kwa vita vya Korea mnamo 1953.

Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono katika mpaka huo.

Kim amesema huu ni ‘mwanzo’ wa amani, baada ya kuvuka eneo la mpaka wa kijeshi unaoigawanya rasi hiyo ya Korea.

Ziara hii inajiri wiki kadhaa baada ya Korea kaskazini kutoa matamshi ya kivita.

Bwana Kim alisema kuwa anatumai kwamba kutakuwa na mazungumzo ya kufana baada ya ufunguzi mzuri wakati mazungumzo hayo yalipoanza.

Mkutano huo wa kihistoria utaangazia maswala ya silaha za kinyuklia na uwezekano wa makubaliano ya amani.

Mengi yatakayozungumzwa ni mambo ambayo tayari yameafikiwa awali lakini wachanganuzi wengi bado wana wasiwasi kuhusu uaminifu wa Korea Kaskazini katika kukubalia kuacha shughuli ya utengezaji wa silaha za kinyuklia.

Hatahivyo shughuli zote za taifa lote la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati ya mpaka wa mataifa hayo mawili.

Na baadaye watu walishangaa baada ya bwana Kim kumualika kiongozi wa Korea Kaskazini kuvuka kwa muda mfupi katika mstari wa mpaka wa mataifa hayo mawili kuingia Korea Kaskazini, kabla ya wawili hao kurudi tena Korea Kusini muda wote huo wakiwa wameshikana mikono.

Kim Jong-un na Moon Jae-in wakipita katika mpaka kati ya mataifa hayo mawili

Viongozi hao wawili walikutana na gwaride ambalo likikuwa limevalia nguo za kitamaduni upande wa taifa la Korea Kusini.

Wawili hao baadaye walielekea katika jumba la amani huko Panmunjom, eneo la kijeshi katika mpaka huo ili kuanza mazungumzo.

Historia mpya imeanza sasa katika mwanzo wa amani, ulisema ujumbe ulioandikwa na bwana Kim alioandika katika kitabu cha wageni ndani ya jumba hilo la amani.

Uzito wa mkutano huo ukiwa ni wa kwanza kati ya viongozi hao wa Korea katika zaidi ya muongo mmoja pia haukukosa ucheshi.

Bwaana Kim alifanya mzaha kuhusu kuleta tambi za baridi katika mkutano huo.

”Nadhani utapendelea sana tambi tulizoleta”, alisema. Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa inatumai kwamba mazungumzo hayo yatapiga hatua.

Mkutano huo wa Korea unaonekana kuwa maandalizi ya mkutano kati ya Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump, mapema mwezi Juni, hatua isiokuwa ya kawaida kwani hakuna rais wa Marekani ambaye aliwahi kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini.

Lengo la mazungumzo

Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kuzungunmzia mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini . Seoul imeonya kwamba kuishawishi Pyongyang kuwacha mpango wake wa kinyuklia itakuwa vigumu .

Teknolojia ya Korea Kaskazini kuhusu silaha za kinyuklia imepiga hatua tangu viongozi wa mataifa hayo mawili kukutana muongo mmoja uliopita. Mkutano huo, ukiwa ni wa tatu kufuatia mikutano mingine iliofanyika 2000 na 2007 unatokana na kuzidi kuimarika kwa uhusiano kati ya mataifa hayo ya Korea.

Kim Jong-un na Moon Jae-in walekeakatika mpaka wa mataifa hayo mawili

Bwana Kim alitangaza wiki iliopita kwamba atasitisha majaribio ya silaha zote za kinyuklia.

Hatua hiyo iliungwa mkono na Marekani na Korea Kusini , licha ya kwamba watafiti wamesema kuwa maeneo ya kujaribu silaha hizo za kinyuklia huenda hayawezi kutumika tena baada ya mwamba kuanguka kufuatia jaribio la mwisho la silaha hizo mwezi Septemba.

Mbali na tangazo la bwana Kim wiki iliopita kwamba atasitisha majaribio ya silaha za kinyuklia , hatua hiyo iliungwa mkono na Marekani na Korea Kusini kama hatua nzuri, ijapokuwa watafiti wa China wamesema kuwa maeneo ya kujaribia silaha hizo hayawezi tena kutumika baada ya mwamba kuanguka Septemba iliopita.

Mbali na hilo viongozi hao wawili pia wanatarajiwa kuzungumzia kuhusu mpango wa amani ili kumaliza vita vya 1950-53 mbali na msururu wa maswala ya kiuchumi na kijamii

Ni nini kitakachofanyika?

KIia maelezo yamepangwa kutoka mpangilio wa mkutano huo hadi chakula kitakachotumika.

Ramani Korea

Baada ya mkutano , wawili hao wataondoka na kupata chakula cha mchana kandokando huku ujumbe kutoka Kaskazini ukielekea katika upande mwengine wa mpaka.

Baada ya sherehe ya mchana , bwana Moon na Kim watapanda mti kwa kutumia udongo na maji kutoka nchi zote mbili ili kuashiria amani.

Raia wa Korea Kusini walijawa na hisia wakati wakitazama muda huo wa kihistoria moja kwa moja katika runinga

Kufuatia kupandwa kwa miti, watatembea kwa pamoja kabla ya kuanza msururu mwengine wa mazungumzo .Mkutano huo utafikia kikomo wakati viongozi hao wawili watakapotia saini makubaliano na kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya chakula cha jioni.

Kim Jong Un ataandaliwa viazi vya kutoka Uswizi ili kumkumbusha wakati wake alipokuwa akisomea nchini Korea Kusini pamoja na chakula cha Korea kaskazini cha tambi baridi na mvinyo wa Korea Kaskazini.

Baada ya chakula cha jioni, ujumbe huo utatazama kanda ya video kwa jina Spring of One kabla ya bwana Kim kurudi nyumbani.

Ni nani atakayehudhuria

Kim anaandamana na maafisa tisa , ikiwemo dadake Kim Yo-jong ambaye aliongoza ujumbe wa Korea Kaskazini katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini mapema mwaka huu.

Kim Yo-jong aliwafurahisha raia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *