KIMBUNGA CHAUA UFILIPINO

KIMBUNGA CHAUA UFILIPINO

Like
243
0
Monday, 24 August 2015
Global News

WAOKOAJI Kaskazini mwa Ufilipino wameendelea na kazi ya kuchimbua ardhini kwa lengo la kutafuta mamia ya wachimba madini waliofukiwa baada ya kukumbwa na kimbunga.

Hali hiyo imekuja kufuatia zaidi ya watu kumi na tano kuripotiwa kufariki dunia na wengine kadhaa hawajulikani walipo kutokana na kimbunga hicho kikubwa.

Hata hivyo mmomonyoko wa udongo ulisababishwa na kimbunga ambacho kilifukia migodi mitatu kaskazini mwa kisiwa cha Luzon ambapo kwa sasa kimepungua kasi na kinaelekea Japan katika kisiwa cha Ryukyu.

Comments are closed.