Kimbunga Michael kuyakumba majimbo matatu Marekani

Kimbunga Michael kuyakumba majimbo matatu Marekani

Like
519
0
Wednesday, 10 October 2018
Global News

Kimbunga Michael: Majimbo matatu kusini mashariki mwa Marekani kuathirika

Takriban watu nusu milioni wanatakiwa kuondoka haraka katika makazi yao eneo la kusini mashariki mwa Marekani ili kukupisha kimbunga Michael ambacho kinakaribia kulikumba eneo hilo.

Taarifa za watabiri wa hali ya hewa zinasema kimbuka hicho kwa sasa kimekwisha ingia katika hatua ya tatu na kuongezeka kasi yake kwa kadri kinavyopitia ghuba ya Mexico kuelekea Jimbo la Florida,Alabama na Georgia.

Kimbunga hicho kinasababisha upepo mkali ambao unakwenda kwa kasi ya kilomita 200 kwa saa,ambapo wataalam wanasema kuwa wakazi wa jimbo la Florida leo huenda watakumbwa na mawimbi maji yatakayotupwa nje na upepo huo kwa kimo cha urefu wa mita tatu jambo ambalo ni hatari hivyo wanatakiwa kuondoka maeneo yanayolengwa na kimbunga Michael.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *