KIPINDUPINDU BADO NI CHANGAMOTO

KIPINDUPINDU BADO NI CHANGAMOTO

Like
197
0
Tuesday, 01 March 2016
Local News

JUMLA ya Wagonjwa wapya 473 wamegundulika kuwa na vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu huku Watu 9 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo katika kipindi cha wiki iliyoanza Februari 22 hadi 28 huku ripoti ikionesha kuwa ugonjwa huo bado umeendelea kusambaa kwa kasi.

Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dokta Hamisi Kigwangala amewata Wananchi kuongeza juhudi za usafi wa afya zao na mazingira kwa kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni za afya.

Katika hatua nyingine dokta Kigwangala amelifungia duka la dawa la Shine care Pharmacy lililopo Temeke Wailes kutokana na kutokuwa na kibali cha kuendesha biashara ya dawa tangu Juni 30 mwaka 2013 na kumtaka Msajili wa Famasia kumpeleka mahakamani mmliki wa duka hilo bwana Mathayo Abraham

Comments are closed.