SERIKALI imesema imedhamiria kuweka mikakati madhubuti itakayowezesha lugha ya Kiswahili kutumika katika ngazi zote nchini ikiwemo utoaji wa hukumu katika mahakama zote ili kuleta haki na usawa kwa wananchi kupitia lugha hiyo.
Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria mheshimiwa UMMY MWALIMU C wakati akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa na mbunge wa viti maalumu mheshimiwa SABRINA SUNGURA ambaye alitaka kujua mikakati ya serikali ya kuhakikisha lugha ya Kiswahili inatumika na kuleta manufaa kwa watu wote.
Hata hivyo akijibu swali hilo katika kipindi cha maswali na majibu mheshimiwa UMMY MWALIMU amesema kuwa katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa kwa kiasi kikubwa ni vyema wananchi wakajitokeza kwa wingi kuipigia kura katiba mpya kwa kuwa imeweka kipaumbele matumizi ya lugha hiyo katika sekta zote kwa manufaa ya Taifa.