WAKAZI WA LINDI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KIJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

WAKAZI WA LINDI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KIJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Like
307
0
Monday, 02 February 2015
Local News

WAKAZI  wa Mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Jerry Silaa  wakati akiongea kwenye kilele cha sherehe za kutimiza miaka 38 ya chama hicho  mkoani Lindi zilizofanyika katika tawi la  Mnazi Mmoja lililopo kata ya Mingoyo wilaya ya  Lindi mjini.

Silaa mbaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala amesema iwapo  mtu atajiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura   atashiriki  katika uchaguzi mkuu ujao hivyo basi wakati ukifika ni jukumu la  mabalozi kuwahimiza  wananchi  kujiandikisha ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Comments are closed.