KOMBE LA DUNIA 2022 KUANZA NOVEMBER MPAKA DECEMBER

KOMBE LA DUNIA 2022 KUANZA NOVEMBER MPAKA DECEMBER

Like
244
0
Tuesday, 24 February 2015
Slider

Kuelekea michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 huko Qatar kikosi maalum cha shirikisho la mpira wa miguu duniani kimetoa mapendekezo ya michuano hiyo kufanyika mwezi wa kumi na moja hadi wa kumi na mbili.

Maofisa hao walikutana huko Doha kujadili mapendekezo kufuatia hofu ya hali ya hewa katika msimu wa kiangazi inaweza kuwaathiri wachezaji na mashabiki.

Msimu wa kiangazi huko Qatar joto huongezeka hadi kufikia nyuzi joto 40C wakati katika kipindi cha November hadi December kiwango hicho hushuka hadi kufikia nyuzi joto 25C.

Mapendekezo hayo ya jumanne yanatarajiwa kuridhiwa na mtendaji wa kamati ya FIFA huko Zurich ifikapo tarehe 19 hadi 20 ya mwezi wa tatu.

Kumekuwa na tetesi zinazodai kuwa michuano hiyo itaanza November 26 na kumalizika December 23, hata hivyo Fifa tayari imesema haina mpango wa kupunguza ukubwa wa michuano kutoka timu 32 au mechi 64

Aidha shirikisho hilo limedai kuwa linapitia maoni mbalimbali kuhusu michuano hiyo

Comments are closed.