Korea kaskazini imefyatua ”kombora” la tatu ndani ya siku 8

Korea kaskazini imefyatua ”kombora” la tatu ndani ya siku 8

Like
889
0
Friday, 02 August 2019
Global News

Korea kaskazini imefyatua kombora la masafa mafupi ambalo halijabainika mara mbili , kwa mujibu wa maafisa wa Korea Kusini , katika jaribio la tatu la silaha hizo katika kipindi cha wiki moja pekee.

Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la mwambao wa mashariki mwa taifa hilo mapema Ijumaa.

hatua hiyo inaonekana kama hatua ya taifa hilo inayolenga kujibu mazoezi ya kijeshi ya baina ya Korea Kusini na Marekani yanayotarajiwa kuanza mwezi huu.

Wakati huo huo Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeitaka Korea kaskazini kushiriki maungumzo ya “maana ” na Marekani.

baada ya mkutano wa faragha katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa , mataifa yalisema kuwa vikwazo vya kimataifa vinapaswa kuimarishwa hadi utawala wa Pyongyang utakapoangamiza mipango yake ya nyuklia makombora ya masafa.

Ufyatuaji wa makombora hayo ulifanyika katika eneo la Yonghung katika jimbo la South Hamgyong katika bahari ya Japan, inayofahamika pia kama Bahari ya Masharik , kwamujibu wa Mkuu wa kikosi cha pamoja cha Korea kaskazini na Korea Kusini (JCS)

Eneo hilo linaonekana kama kituo cha kufyatulia makombora ambacho hakijawahi kutumiwa awali , amesema Ankit Panda, afisa katika shirikisho la wanasayansi wa Marekani – Federation of American Scientists.

“Hiki ni kielelezo kingine cha enzi ya Kim Jong-un zaidi ya ufyatuaji wa makombora ya usiku : kufyatua kutoka vituo ambavyo havikuwahi kutumiwa awali au ambavyo havitumiwi .”

Akizungumza katika ikulu ya White House, rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hana hofu na ufyatuaji wa hivi karibuni w amakombora kwasababu ni ya masafa mafupi na “ni ya kiwango cha kawaida “.

Vipi kuhusu majaribio mengine?

Jumatano , Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa yanayopaa kilomita 250 (maili 155 ) na kufikia urefu wa kilomita 30 kabla ya kutua kwenye bahari ya Japan, inayofahamika a Bahari ya mashariki , k wamujibu wa Korea Kusini.

Korea Kusini iliyatambua makombora hayo ya masafa kuwa yalikuwa ni aina tofauti na yaliyofyatuliwa awali . Lakini Alhamisi , Pyongyang ilitoa kauli tofauti , ikisema kuwa ilifanya majaribio ya mfump mpya wa ufyatuzi wa roketi, lakini haikutoa maelezo.

Mnamo Julai 25, Korea kaskazini ilifyatua makombora mengine mawili, moja likiwa na uwezo wa kusafiri takriban kilomita 690.

Ufyatuaji huo wa makombora ulikuwa ni wa kwanza kufanyika tangu Bwana Trump na kiongozi wa korea Kim Jong-un wafanye mkutano ambao haukupangwa mwezi Juni katika eneo lisilokuwa na silaha ,, ambalo linatenganisha Korea mbili , ambako walikubaliana kuanzisha mazungumzo ya kuacha matumizi ya nyuklia.

Ni nini kinachoendelea sasa?

Korea kaskazini hivi karibuni ilipaza sauti ya hasira yake dhidi ya mazoezi yaliyopangwa kufanyika baina ya Marekani na Korea Kusini, tukio la mwaka ambalo washirika wamekataa kuachana nalo ,lakini limeleta athari kubwa.

Korea kaskazini inayaona mazoezi hayo ya kijeshi lama maandalizi ya vita na iliyaita “uvuriugaji wa roho ” wa kauli ya pamoja aliyoisaini Bwana Trump na Kim katika kikao chao cha kwanza cha ana kwa ana cha mwaka jana cha Singapore.

Pyongyang ilikuwa imeonya kwamba mazoezi hayo yanaweza kuathiri kufufuliwa kwa mazungumzo ya kuanchana na nyuklia.

Jumatatu waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alisema kwamba anatumaini mazungumzo haya yanaweza kuanza “haraka sana ”, lakini hakuna mkutano uliopangwa.

Mwaka jana , Bwana Kim alisema Korea Kaskazini ingesitisha majaribio ya nuklia, na ingeacha kufyatua tena makombora ya masafa marefu yanayoweza kuvuka mipaka ya mabara.

Shughuli za nyuklia zinaelekea kuendelea, hata hivyo , na picha za setilaiti za kituo kikuu cha nyuklia cha Korea Kaskazini mwezi uliopita zilionyesha kuwa taifa hilo huenda linatengeneza mionzi ya inayochochea makombora.

Serikali ya Pyongyangpia inaendelea kuonyesha uwezo wake wa kutengeneza silaha mpya licha ya kuwekewa vikwazo vikali vya kiuchumi.

Ilifyatua kombora la masafa mafupi la aina hiyo mapema mwezi Mei ,likiwa ni kombora la kwanza la aina yake tangu iliporusha kombora la ballistic mnamo mwaka 2017.

Korea Kaskazini pia ilionyesha manuwari yake ya kijeshi wiki iliyopita, ambayo maafisa wa Korea Kusini wamesema ina uwezo wa kubeba makombora hadi matatu ya masafa ya ballistic.

cc;BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *