KUBENEA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI MITATU KWA KUMTUSI PAUL MAKONDA

KUBENEA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI MITATU KWA KUMTUSI PAUL MAKONDA

Like
372
0
Thursday, 14 April 2016
Local News

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia chama cha (CHADEMA) Saeed Kubenea kifungo cha nje cha miezi mitatu kutokana na kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

 

Akisoma hukumu hiyo jana Jijini Dar es Salaam Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu Thomas Simba amesema kuwa mahakama imeamua kumpa mshitakiwa adhabu ya kifungo hicho kwa kuwa ndilo kosa lake la kwanza, hivyo Mshitakiwa anastahili kupata adhabu ya huruma.

 

Adhabu hiyo iliyotolewa chini ya kifungu namba 89, kifungo kidogo cha kwanza Mheshimiwa Kubenea hatakiwi kufanya kosa la aina yoyote ambalo litamsababisha arudishwe tena mahakamani na endapo itatokea akafanya hivyo mahakama itampa adhabu ya kifungo cha kwenda jela.

Comments are closed.