MJADALA: JE NINI KIMEBADILIKA WAKATI HUU HADI WASANI KUFUNGIWA NYIMBO ZAO?
INSPECTA HAROUN: aa labda niseme kitu kimoja, dunia siku hizi ni kama kijiji, Haikwepeki kulinda Utamaduni wetu
INSPECTA HAROUN: Kwenye nyimbo ambazo zimefungiwa zingine kiukweli hazikustaili na zingine zina staili
NIKI WA PILI: Nakumbuka Mziki wa enzi zile ulikuwa na kama uhuni hivi
NIKI WA PILI: namkumbuka professor mmoja alisema mziki wetu ni sehemu ya kuvumbua maovu.
NIKI WA PILI: Kufungiwa kwa hizi nyimbo kuna vitu vingi tunatakiwa tuvijadili sana tena kwa kina
INSPECTA HAROUN: Unajua hata huko Basata kwenyewe hakuna watu ambao wanujua mziki, ila hatuwezi kuwasema sana hapa hewani
NIKI WA PILI: kuna mikanganyiko, uwazi kipindi cha uchaguzi kwenye kampeni 2015 kuna nyimbo zilitumika hazikuwa na maadili
INSPECTA HAROUN: Mtoto ameamua kusimama mwenyewe kwa hiyo baba akimrudi mtoto basi anapaswa kumrudia kwa kumfundisha sio mkomoa
NIKI WA PILI: Basata ilikuwepo hata kabla ya sisi, kwa hiyo sisi ni tunafanya biashara, lakini Basata wapo kwa ajili ya kulinda Maadili.
INSPECTA HAROUN: Kama sisi wasanii hatuja kaa pamoja na Basata na kila mmoja akatoa duku duku lako, alafu na serikali ikikaa na Basata mimi nafikili hakuta kuwa na mkanganyiko kama huu