LIBYA: BUNGE LAKATAA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

LIBYA: BUNGE LAKATAA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Like
169
0
Tuesday, 20 October 2015
Global News

BUNGE la Libya linalotambulika na Jumuiya ya kimataifa limeyakataa mapendekezo ya Umoja wa Mataifa ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

Mbali na hayo Baraza hilo la wawakilishi limesema kuwa litashiriki mazungumzo ya Amani ya Umoja wa Mataifa pamoja na mahasimu wao wanaoendesha serikali nyingine kutokea mji mkuu wa Tripoli.

Hata hivyo Mataifa ya Magharibi yanazishinikiza pande mbili kuyaafiki makubaliano ya Umoja wa Mataifa, miaka minne tangu kuangushwa na kuuawa kwa kiongozi wa muda mrefu wa Taifa hilo Muammar Ghadhafi.

 

Comments are closed.