Libya yaweka saini kusitisha mapigano

Libya yaweka saini kusitisha mapigano

Like
677
0
Wednesday, 05 September 2018
Global News

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa ulioko nchini Libya umetangaza mkataba wa kusitisha mapigano ambao umeafikiwa baina ya pande mbili ule wa serikali na viongozi wa kijeshi mjini Tripoli, pamoja na viongozi wa vikundi vidogo vyenye silaha nchini humo.

Tangazo hilo limekuja baada ya siku nane za mapigano makali baina ya wanamgambo wa wapiganaji wanaohusishwa na mamlaka ya kimataifa kutambuliwa katika mji mkuu wa Libya na wengineo kutoka nje ya mji mkuu.

Hili ni jaribio la tatu kufikiwa katika harakati za kujaribu kumaliza mapigano na vurugu na ukatili mjini Tripoli.Majaribio ya awali ya kumaliza mapigano yalikufa mara baada tu ya kufikiwa.

Wakati huu utiwaji saini wa makubaliano ya kumaliza mapigano kumeidhinishwa na umoja wa mataifa, miongoni mwa makubaliano ni kukomesha maadui wote, kuwalinda raia na ombi la kufunguliwa kwa uwanja mkuu wa ndege ulioko mjini Tripoli, ambao ulifungwa siku nne zilizopita kutokana na ghasia na mapigano.

Haijawa wazi mpaka sasa juu ya taarifa za kina juu ya kile kilichoridhiwa katika makubaliano hayo ya kusitisha mapigano ingawa vikundi vidogo vidogo vyenye silaha vilivyoshiriki katika siku nane za mapigano makali , kimetoa taarifa kuwa kamanda wa vikosi vyao anaunga mkono suluhu.

Kikundi hiki kinadai kwamba makubaliano ni pamoja na kuondoka kwa wapinzani wake kutoka mji mkuu wa Libya.

Wapinzani hao ni vikosi vya kijeshi ambavyo vinahusishwa na wizara ya mambo ya ndani ya serikali ya Tripoli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *