LOWASA AKARIBISHWA RASMI UKAWA

LOWASA AKARIBISHWA RASMI UKAWA

Like
284
0
Monday, 27 July 2015
Local News

UKAWA umetangaza rasmi kumkaribisha waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa kuungana na Umoja huo nakusema kuwa wapo tayari kushirikiana naye na kumpa nafasi. Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NCCR –Mageuzi Mheshimiwa James Mbatia amesema Ukawa wanamkaribisha na yuko huru kuamua chama anachotaka kuungana nacho. Tamko hili la leo limekuja baada ya kuwepo na vuta nikuvute katika vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi , kuhusu kukubaliwa au kutokubaliwa kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa kujiunga na umoja huo, na taarifa za ndani zinaeleza kuwa ataungana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA.

IMG-20150727-WA0091

Comments are closed.