LUBUVA: TUME INAFANYA KAZI ZAKE KWA TARATIBU ILIZOJIWEKEA NA SIO MATAKWA YA MTU BINAFSI

LUBUVA: TUME INAFANYA KAZI ZAKE KWA TARATIBU ILIZOJIWEKEA NA SIO MATAKWA YA MTU BINAFSI

Like
284
0
Tuesday, 27 October 2015
Local News

KUFUATIA uwepo wa mitazamo tofauti kwa tume ya Taifa ya uchaguzi kuhusu kupendelea upande mmoja wakati wa utangazaji wa matokeo, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema Tume inafanya kazi zake kwa mujibu wa utaratibu iliyojiwekea na sio kwa matakwa ya mtu binafsi.

Aidha Jaji mstaafu Lubuva amesema kuwa matokeo ya ngazi ya urais kutoka majimbo ya uchaguzi kote nchni hutangazwa kwa wananchi kwa kadiri yanavyo pokelewa na sio vinginevyo.

Hata hivyo amesema kuwa hali hiyo imesababishwa na ucheleweshwaji wa uwasilishwaji wa taarifa za matokeo kutoka katika vituo vya uchaguzi na kuwataka maafisa wa uchaguzi kuharakisha matokeo ili tume hiyo iweze kuyatangaza haraka.

Comments are closed.