Maafisa wa zamani wa serikali matatani Sudan

Maafisa wa zamani wa serikali matatani Sudan

Like
682
0
Monday, 15 April 2019
Global News

Baraza la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji.

Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumuidhinisha watakayemchagua.

Maandamano ya miezi kadhaa nchni Sudan yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi wa muda mrefu nchini Sudan Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita

Waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia

Raia wanaendelea kuandamana na wamekita kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu Khartoum.

Katika mkutano na waandishi habari siku ya Jumapili, msemaji Meja Jenerali Shams Ad-din Shanto ameeleza kwamba baraza la kijeshi lipo “tayari kuidhinisha” serikali yoyote ya kiraia itakayoidhinishwa na vyama vya upinzani.

“Hatutomteua waziri mkuu. Watamchagua,” alisema akimaanisha upinzani na makundi yanayoandamana.

Ameeleza pia kwamba jeshi halitowaondoa waaandamanaji kwa lazima lakini ametoa wito kwa waandamanaji hao “kuruhusu maisha yaendelee kama kawaida” na waache kuweka vizuzi kinyume cha sheria.

“Kushika silaha hakutoruhusiwa,” aliongeza

Maandamano ya kupinga kupanda gharama ya maisha yalianza Desemba mwaka jana lakini punde tu yakageuka kuwa wito mkubwa wa kumpinga rais bashir na utawala wake.

Aliyeongoza mapinduzi hayo, waziri wa ulizni Awad Ibn Auf, alitangaza kwamba jeshi litasimamia serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka miwili kitakachofuatwa kwa uchaguzi na akaidhinisha miezi mitatu ya hali ya dharura.

Lakini wandamanji waliapa kusalia mitaani hata baada ya hatua hiyo, wakitaka maguezi na kuidhinishwa kwa serikali ya kiraia mara moja.

A Sudanese girl flashes the victory sign and holds the national flag during a rally near the military headquarters in the capital Khartoum on April 11, 2019. – The Sudanese army is planning to make “an important announcement”, state media said today, after months of protests demanding the resignation of longtime leader President Omar al-Bashir. Thousands of Khartoum residents chanted “the regime has fallen” as they flooded the area around army headquarters where protesters have held an unprecedented sit-in now in its sixth day. (Photo by – / AFP)-/AFP/Getty Images

Ibn Auf himself alijiuzuliu ziku ya pili , kama alivyojiuzulu mkuu wa usalama anayeogopwa na wengi Jenerali Salah Gosh.

Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan baada ya hapo alitajwa kuwa kiongozi wa baraza la mpito la kijeshi, kuwa kiongozi wa tatu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha siku nyingi.

Lakini muungano wa wataalamu Sudan (SPA), ambao umekuwa ukiongoza maandamano hayo umesema muitikio wa baraza hilo “haukudhihirisha matakwa yoyote ya raia” na ametaka maandamano yaendelee.

Miongoni mwa matakwa yao ni kutaka idara ya ulinzi ifanyiwe mageuzi, “viongozi wafisadi” wakamatwe na kuvunjiliwa mbali makundi ya sungusungu yaliohudumu chini ya rais wa zamani Bashir.

Kiongozi huyo wa zamani hajulikani yuko wpai, lakini viongozi wa mapinduzi hayo wanasem ayumpo mahali salama.

Bashir ameshtakiwa kwa mashtaka ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binaadamu huko Darfur na mahakama ya kimatiafa ya jinai ICC.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *