MACHAFUKO: RAIA WA MAREKANI KUONDOKA BURUNDI

MACHAFUKO: RAIA WA MAREKANI KUONDOKA BURUNDI

Like
232
0
Monday, 14 December 2015
Global News

SERIKALI ya Marekani imeshauri Raia wake walio nchini Burundi kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo baada ya watu 87 kuuawa kwenye ghasia zilizotokea siku ya Ijumaa.

 

Ghasia zilizojitokeza kwenye mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura ni mbaya zaidi tangu kuanza kwa vurugu mwezi Aprili mwaka huu , baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.

 

Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch (HRW) limeitisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo ya Ijumaa.

Comments are closed.