MACHAR AREJEA SUDAN KUSINI

MACHAR AREJEA SUDAN KUSINI

Like
275
0
Wednesday, 13 April 2016
Local News

KIONGOZI wa waasi nchini Sudan Kusini, Riek Machar, amerejea nchini humo kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili kama sehemu ya utekelezwaji wa mkataba wa amani.

Atakapowasili mjini Juba, Bwana Machar anatarajiwa kuchukua wadhfa wake wa makamu wa rais.

Msemaji wake amethibitisha kwamba bwana Machar alikuwa katika makao makuu ya waasi yaliyo katika mji wa Pagak mpakani na taifa jirani la Ethiopia.

Comments are closed.