MADEREVA WA TANZANIA KUZUILIWA KUBEBA WATALII KENYA !!!

MADEREVA WA TANZANIA KUZUILIWA KUBEBA WATALII KENYA !!!

Like
363
0
Thursday, 05 February 2015
Local News

WIZARA ya Maliasili na Utalii imetakiwa kuchukuwa tahadhari kubwa katika kufatilia sakata la Madereva wa Tanzania kuzuiliwa kubeba Watalii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata nchini Kenya ili kunusuru Mapato ya Taifa yanayoweza kupotea kupitia biashara ya utalii.

Tahadhari hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Uchukuzi SAMWEL SITA alipotakiwa na Spika wa Bunge ANNE MAKINDA kutoa ufafanuzi juu ya Sakata hilo katika kipindi cha Maswali na Majibu ambapo amesema   Kenya inaweza kuipunguzia Nchi mapato kwa kutaka Watalii walale kwenye hoteli za Kenya na kufanya Utalii Tanzania.

Waziri Sita amesema ili Tanzania ifaidike na biashara ya Utalii ni lazima ihakikishe Watalii wanatembelea vivutio vilivyopo nchini na kulala katika hoteli zilizopo nchini badala ya kuzifaidisha hoteli za Kenya kupitia vivutio vilivyopo nchini.

 

Comments are closed.