MAELFU WAMUAGA PAPA WEMBA KINSHASA:

MAELFU WAMUAGA PAPA WEMBA KINSHASA:

Like
238
0
Tuesday, 03 May 2016
Global News

Maelfu ya waombolezaji walijitokeza kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba.
Waomboloezaji walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast.
Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa.
Serikali imetangaza siku tatu za maombolezi kuanzia leo hadi jumatano atakapozikwa.
Tayari amepewa tuzo kwa mchango wake.
Msanii huyo nguli alikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano.
Wengi waliitambua sauti hiyo ya na utunzi wake.
Alikuwa ni mtumbuizaji kamili.

Gwiji huyo wa muziki wa Lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu – Wilaya ya Sankuru nchini Congo.
Jina lake halisi ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba.
Yeye alianza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.

Alikuwa akimfuata mamake katika matanga na hivyo akaibukia kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza.
Mfalme huyo wa muziki wa Rhumba, mwenye umri wa miaka 66 aliaga dunia ghafla 24 April akiwa nchini Ivory Coast .

Comments are closed.