MAELFU YA WAHAMIAJI WASUBIRI KUINGIA ULAYA

MAELFU YA WAHAMIAJI WASUBIRI KUINGIA ULAYA

Like
179
0
Thursday, 03 September 2015
Global News

SWALA la wakimbizi na wimbi la wahamiaji katika nchi za ulaya linaendelea kutazamwa kwa karibu wakati maelfu ya watu wakisubiri kuruhusiwa kuingia katika nchi za jumuia ya ulaya.

Na siku ya jana hali ilikuwa ya kusikitisha baada ya picha ya kijana aliyezama kuonekana akiwa katika pwani ya Bahari nchini Uturuki kusambaa katika mitandao ya kijamii.

Waziri mkuu wa uingereza David Cameron alitetea uamuzi wa serikali yake akisema kuwa kuwapokea watu zaidi siyo ufumbuzi wa tatizo.

Badala yake, amesema ni muhimu kuhakikisha amani na utulivu vinakuwepo katika maeneo ambayo wahamiaji wanatoka, kama vile Syria.

Comments are closed.