MAFUA YA NDEGE TENA UINGEREZA

MAFUA YA NDEGE TENA UINGEREZA

Like
272
0
Monday, 17 November 2014
Global News

MLIPUKO wa Mafua ya Ndege umethibitishwa katika Shamba moja la kuzalishia Bata Mashariki mwa Yorkshire, nchini Uingereza, wamesema maafisa.

Wizara ya Mazingira, Chakula na Masuala ya Vijijini -DEFRA imesema kuwa Mafua ya Ndege hatari yake ni ndogo sana kwa Afya ya umma.

Taarifa zaidi zimebainisha kuwa Ndege wasiohitajika wanatakiwa kuondolewa kutoka eneo hilo na kuwaweka sehemu maalum ambayo itakuwa imeandaliwa.

Tatizo hilo bado halijathibitishwa, lakini aina ya Kirusi cha H5N1 hakijaweza kubainishwa na maafisa wa DEFRA.

Comments are closed.