MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA LEO

MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA LEO

Like
767
0
Tuesday, 24 November 2015
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania na kuzungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.

 

Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais ameueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya mama na mtoto, elimu na mazingira.

 

Kuhusu Afya ya mama na mtoto Mheshimiwa Suluhu amesema kazi hiyo ataianza hivi karibuni kwa kushirikiana na Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki za wanawake ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na mimba za utotoni.

MAK32 MAK21

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea baadhi ya Vipeperushi na Vitabu vya Mtandano wa Wanawake Tanzania (WFT) kutoka kwa mwenyekiti wa mtandao huo, Prof.Ruth Meena, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dares Salaam

Comments are closed.