MAKAPU YA SIKUKU HAYABEBEKI YALIVYOSHEHENI MAZAGAZAGA

MAKAPU YA SIKUKU HAYABEBEKI YALIVYOSHEHENI MAZAGAZAGA

Like
631
0
Thursday, 24 December 2015
Entertanment

Kituo bora cha radio 2015 E-fm leo kimekabidhi zawadi ya makapu yaliyosheheni bidhaa za vyakula kuelekea sikukuu ya Christmas

Zoezi hili liliwataka wasikilizaji wa E-fm kusikiliza mlio wa Jingle Bells uliokuwa ukizunguka kwenye vipindi tofauti kisha kutambua muda ambao mlio huo umesikika, jina la kipindi husika na mtangazaji/watangazaji wa zamu waliokuwa studio muda huo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi makapu hayo kwa washindi Meneja wa vipindi E-fm Bwana Dickson Ponela (Big Dad Dizzo) ameeleza kuwa, E-fm imekuwa ikishirikisha wasikilizaji wake kwa kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwemo kuwawezesha kimaisha kama  sehemu ya shukrani kwa kuichagua E-fm

1

Meneja wa vipindi E-fm Dickson Ponela akiwaonyesha washindi makapu ya sikukuu

2

Uzito wa kapu la sikukuu sio kazi rahisi kubebwa na mtu mmoja msaada muhimu

3

Watatu kutoka kulia ni Dickson Ponela, wa kwanza kushoto ni Sendo kwenye picha ya pamoja na baadhi ya washindi

4

Kaimu Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja NIC bwana Elisante Maleko akikabidhi kapu kwa mtoto Steve mkazi wa Kimara Suka aliyejishindia kapu la sikukuu

5

Lukia mshindi kutoka Mabibo akipakia kapu lake kwenye Bodaboda tayari kuanza safari

6

Patric Boniface kutoka Goba aliyeambatana na baba yake wakipakia mzigo wao kwenye bodaboda

7

Mama Pili kutoka Gobgo la Mboto akipakia kapu lake kwenye Bajaji

8

Comments are closed.