MAKONDA AWEKA MAWE YA MSINGI YA UJENZI WA SHULE 2 ZA SEKONDARI KINONDONI

MAKONDA AWEKA MAWE YA MSINGI YA UJENZI WA SHULE 2 ZA SEKONDARI KINONDONI

Like
697
0
Monday, 11 January 2016
Local News

KATIKA kupunguza tatizo la watoto wengi wanaomaliza darasa la saba kushindwa kuendelea na elimu ya Sekondari kutokana na uhaba wa Madarasa wilayani Kinondoni , Mkuu wa Wilaya hiyo,  Paul Makonda leo ameweka mawe ya msingi ya ujenzi wa shule za Sekondari Mbezi Juu na shule ya Sekondari Mzimuni zinazojengwa katika manispaa ya Kinondoni.

 

Akizungumza na Waandishi wa habari pamoja na wananchi wakati akiweka mawe hayo ya msingi Makonda amesema hii ni sehemu yamkakati wa Manispaa hiyo kujenga shule za Sekondari zipatazo saba katika Manispaa ya Kinondoni ili kumaliza tatizo wa wanafunzi kutoendelea na shule ya sekondari ambapo sasa  vinajengwa vyumba vine vya Madarasa Mbezi juu na vyumba sita kwa upande wa Mzimuni

Screenshot_2016-01-11-11-18-45

Comments are closed.