MALAYSIA: KIONGOZI WA UPINZANI APIGWA MIAKA 5 JELA KWA KOSA LAKULAWITI

MALAYSIA: KIONGOZI WA UPINZANI APIGWA MIAKA 5 JELA KWA KOSA LAKULAWITI

Like
343
0
Tuesday, 10 February 2015
Global News

MAHAKAMA ya juu nchini Malaysia leo imethibitisha hukumu ya awali dhidi ya kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim kwa kosa la kufanya  mapenzi na mwanamme mwenzake, kesi inayoangaliwa nje na ndani ya nchi hiyo kuwa ni njama ya kisiasa kumaliza  mwanasiasa huyo ambaye ni kitisho kwa serikali.

Jaji wa mahakama ya Shirikisho Arifin Zakat amesema  madai ya  msaidizi wa Anwar kuwa alimtongoza  na kuwa na uhusiano naye yana uzito na kwamba hukumu ya kifungo cha miaka mitano jela iliyopitishwa na mahakama ya rufaa mwaka jana ni sahihi.

Kushindwa kwa rufaa yake, kunamaanisha kuwa kiongozi huyo wa upinzani anarudi tena gerezani.

150210104400_cn_putrajaya_anwar_03_512x288_afp_nocredit

Comments are closed.