MALAYSIA YASITISHA SHUGHULI YA UTAFUTAJI WA NDEGE YA MH370

MALAYSIA YASITISHA SHUGHULI YA UTAFUTAJI WA NDEGE YA MH370

Like
281
0
Thursday, 29 January 2015
Global News

SERIKALI ya Malaysia imesitisha shughuli ya kuitafuta ndege ya iliyopotea ya MH370 na kuitaja kama ajali huku ikisema hapakuwa na manusura wa ajali hiyo.

Maafisa wakuu wanasema shughuli ya kuipata ndege hiyo, bado inaendelea lakini inasemekana abiria 239 waliokuwa kwenye ndege hiyo walifariki.

Ndege hiyo bado haijulikani iliko na wala kujulikana ilikopotelea licha ya shughuli kubwa ya kimataifa kuitafuta kusini mwa bahari ya hindi.

Tangazo la serikali ya Malaysia, lililotolewa leo, linatoa fursa kwa jamaa wa waathiriwa wa ajali hiyo kulipwa fidia.

 

Comments are closed.