MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA

MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA

Like
481
0
Friday, 12 December 2014
Local News

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa –NEC, ya Chama Cha Mapinduzi –CCM, kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika  uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea na wanachama pamoja na wagombea wa nafasi za Uenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata za Ndoro na Mikumbi zilizopo wilaya ya Lindi mjini.

Amesema kuna baadhi ya watu hawajiandikishi na wengine siku ya uchaguzi ikifika hawaendi kupiga kura, na badala yake wanabaki kulalamika viongozi hawafai, hivyo amewataka washiriki katika uchaguzi na kuhakikisha wamechagua viongozi wanaowataka.

 

Comments are closed.